Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 8:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Akageuka akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akinena, Enenda zako nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, hali ya wana Adamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema, “Ondoka mbele yangu Shetani! Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema, “Ondoka mbele yangu Shetani! Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema, “Ondoka mbele yangu Shetani! Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Lakini Isa akageuka na kuwaangalia wanafunzi wake, na akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Lakini Isa alipogeuka na kuwaangalia wanafunzi wake, akamkemea Petro. Akasema, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

Tazama sura Nakili




Marko 8:33
24 Marejeleo ya Msalaba  

Nae hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakinena. Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.


Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu.


Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.


Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akanena, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu.


Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:


Bwana akageuka, akamtazamisha Petro: Petro akalikumbuka neno la Bwana, jinsi alivyomwambia, Kabla hajawika jogoo leo, utanikana marra tatu.


Yesu akamwambia, Nenda zako nyuma yangu, Shetani: maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.


Akageuka, akawakaripia, akasema, Hamjui ni moyo wa namna gani mlio nao.


kumtolea Shetani mtu huyo, mwili uadhibiwe, illi roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.


mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.


Wale watendao dhambi, uwakemee mbele ya watu wote, illi na wengine waogope.


Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali wapate uzima katika Imani,


BASSI kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake kwa ajili yenu, ninyi nanyi jivikeni nia ile ile kama silaha; kwa maana yeye allyeteswa katika mwili, ameachana na dhambi;


Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.


Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo