Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 8:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Wakatokea Mafarisayo wakaanza kuhujiana nae; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka afanye ishara kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka afanye ishara kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka afanye ishara kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Isa. Ili kumtega, wakamwomba awaoneshe ishara kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Isa. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili




Marko 8:11
27 Marejeleo ya Msalaba  

Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakinena, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.


Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je, ni halali mtu kumwacha mkewe kwa killa sababu?


Hatta alipokwisha kuingia hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakinena, Kwa mamlaka gani unafanya haya? Na nani aliyekupa mamlaka haya?


Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafauya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno.


Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki?


Siku ile Masadukayo, watu wanenao kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,


Nae, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? nileteeni dinari niione. Wakaleta.


Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Akawauliza wale waandishi, Nini mnajadiliana nao?


Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele?


Wengine kwa kumjaribu wakataka ishara ya mbinguni.


Bassi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa.


Wakamwambia, Unafanya ishara gani bassi illi tuone tukaamini? Unatenda kazi gani?


Ni nani katika wakubwa amwammiye, au katika Mafarisayo?


Wakasema neno hili wakimjaribu wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika inchi.


Petro akamwambia, Hikuwaje hatta mkapatana kumjaribu Roho ya Bwana? angalia, miguu yao waliomzika mume wako ipo mlangoni, nao watakuchukua wewe nawe.


Wala tusimjaribii Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo