Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 7:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Effatha, maana yake, Funguka!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, “Efatha,” maana yake “Funguka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, “Efatha,” maana yake “Funguka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, “Efatha,” maana yake “Funguka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Ndipo Isa akatazama mbinguni, akashusha pumzi kwa nguvu, akamwambia, “Efatha!” (yaani, “Funguka!”)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Ndipo Isa akatazama mbinguni, akavuta hewa ndani kwa nguvu akamwambia, “Efatha!” Yaani, “Funguka!”

Tazama sura Nakili




Marko 7:34
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.


Na saa tissa Yesu akapiga kelele kwa sauti kuu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? tafsiri yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?


Akamshika mkono yule kijana, akamwambla, Talitha, kumi: tafsiri yake, Kijana, nakuambia, Ondoka.


Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote.


Marra masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.


Akaugua rohoni mwake, akanena, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.


Yesu akamwambia, Upewe kuona imani yako imekuponya.


Nae alipokaribia akauona mji, akaulilia,


Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka.


Bassi, Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana nae wanalia, akaugua rohoni, akajifadhaisha nafsi yake,


Yesu akatoka machozi.


Bassi Yesu akiugua tena nafsini mwake akatika kaburini. Nalo lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.


Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.


Akiisha kusema haya, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, toka, njoo huku.


MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe;


Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya: ondoka, ukatandike kitanda chako.


Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo