Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 6:48 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

48 Akawaona wakitaahika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hatta yapata zamu ya nne ya usiku akawaendea akitemhea juu ya bahari; akataka kuwdpita.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

48 Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,

Tazama sura Nakili

Marko 6:48
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.

Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angalijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.

Kesheni bassi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au usiku wa manane, au awikapo jogoo, an assubuhi:

Ilipokuwa jioni chombo kilikuwa kati ya bahari, na yeye peke yake katika inchi kavu.

Nao walipomwoua anatembea juu ya bahari walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe, kwa sababu wote walimwona, wakafadhaika.

Na akija kesha la pili au akija kesha la tatu, na kuwakuta hivi, wa kheri watumishi wale.

Wakakikaribia kijiji walikokuwa wakienda; nae akajifanya kama anataka kwenda mbele.

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo