Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 6:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akaimega mikate, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu. Na wale samaki wawili pia akawagawia wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili.

Tazama sura Nakili

Marko 6:41
22 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akamega, akawapa wanafunzi ile mikate, wanafunzi wakawapa makutano.

akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.

Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ni mwili wangu.

Nao wakila, akatwaa mkate, akahariki, akamega, akawapa, akasema, Twaeni; huu ni mwili wangu.

Wakaketi kwa safu, nyingine mia, nyingine khamsimi.

Wakala wote wakashiba.

akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Effatha, maana yake, Funguka!

Nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Thenashara.

Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia.

Wakafanya hivi, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi, kuviweka mbele ya makutano.

Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe;

Bassi Yesu akaitwaa mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.

(lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru);

Alipokwisha kusema haya akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula.

Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.

Bassi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo