Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 6:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Mfalme Herode akasikia khabari; kwa maana jina lake limepata kutangaa, akanena, Yohana Mbatizaji amefufuka, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Wengine walinena, Yu Eliya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, mfalme Herode alisikia juu ya hayo yote, maana sifa za Yesu zilienea kila mahali. Baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohane Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu, ndiyo maana nguvu hizi zinafanya kazi ndani yake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, mfalme Herode alisikia juu ya hayo yote, maana sifa za Yesu zilienea kila mahali. Baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohane Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu, ndiyo maana nguvu hizi zinafanya kazi ndani yake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, mfalme Herode alisikia juu ya hayo yote, maana sifa za Yesu zilienea kila mahali. Baadhi ya watu walikuwa wakisema, “Yohane Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu, ndiyo maana nguvu hizi zinafanya kazi ndani yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Isa lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yahya amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Isa lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yahya amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

Tazama sura Nakili

Marko 6:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wakatoka, wakaeneza khabari zake katika inchi ile yote.

Khahari zake zikaenea marra inchi zote kando ya Galilaya.

Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali.

Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine Eliya; wengine mmojawapo wa manabii.

Siku ile ile baadhi ya Mafarisayo wakamwendea, wakamwambia, Ondoka hapa, ukaende zako: kwa maana Herode anataka kukuua.

HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,

Zikatoka hizo khabari zake katika Yahudi yote, na katika inchi yote iliyozunguka.

Wakajibu, wakasema, Yohana Mbatizaji: na wengine, Eliya: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka.

Maana kutoka kwenu Neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu: bali na katika killa mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea, hatta hatuna haja sisi kunena lo lote.

Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo