Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 5:40 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

40 Nae alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa baba yake yule mtoto na mama yake, na wale walio pamoja nae, akaingia ndani alimokuwamo yule mtoto.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Lakini wao wakamcheka. Basi, akawatoa wote nje, akawachukua baba yake na mama yake huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Lakini wao wakamcheka. Basi, akawatoa wote nje, akawachukua baba yake na mama yake huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Lakini wao wakamcheka. Basi, akawatoa wote nje, akawachukua baba yake na mama yake huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Wale watu wakamcheka. Baada ya kuwafukuza wote nje, Isa akaenda na baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaingia ndani hadi pale alipokuwa mtoto yule.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Wale watu wakamcheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto.

Tazama sura Nakili

Marko 5:40
14 Marejeleo ya Msalaba  

Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu.

Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararueni.

Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana.

Akamshika mkono yule kijana, akamwambla, Talitha, kumi: tafsiri yake, Kijana, nakuambia, Ondoka.

Mafarisayo nao wakayasikia haya yote, nao walikuwa wakipenda fedha; wakamdhihaki.

Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo