Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 4:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Siku ile ilipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke ziwa, twende ngambo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke ziwa, twende ngambo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke ziwa, twende ng'ambo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Ilipokaribia jioni ya siku hiyo, Isa akawaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Siku hiyo ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni twende mpaka ng’ambo.”

Tazama sura Nakili




Marko 4:35
11 Marejeleo ya Msalaba  

Marra Yesu akawalazimisha wamifunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ngʼambu, wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.


Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, akaamuru kuvuka hatta ngʼambu.


Hatta Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ngʼambu katika kile chombo, wakamkusanyikia makutano mengi: nae alikuwa kando ya bahari.


Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.


Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hatta ngʼambu.


Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga.


Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakastaajabu, wakasemezana, Huyu ni nani, bassi, kwa kuwa hatta upepo na bahari aviamuru vikamtii?


BAADA ya haya Yesu alikwenda zake ngʼambu ya bahari ya Galilaya, bahari ya Tiberia.


wakapanda chomboni wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaum. Na giza imekwisha kuwa, nae Yesu hajawafikia.


Hatta walipomwona ngʼambu ya bahari, wakamwambia, Rabbi, umekuja lini hapa?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo