Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Isa akawatazama kwa hasira watu waliomzunguka pande zote, akahuzunika sana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa umeponywa kabisa!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Isa akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa kabisa!

Tazama sura Nakili




Marko 3:5
29 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, nkawa mzima kama mkono wa pili.


Akawaambia, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? Wakanyamaza.


Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha?


Alipowaona, akawaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa katika kwenda kwao wakatakasika.


Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako.


akampaka kipofu macho kwa lile tope, akamwambia, Enenda, kanawe katika birika ya Siloam (tafsiri yake, Aliyetumwa). Bassi akaenda, akanawa, akarudi, anaona.


Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili;


pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo;


akili zao zimetiwa giza, wamekaa mbali na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo niwao, kwa sababu mioyo yao imekufa ganzi:


Mwe na ghadhabu, wala msifanye dhambi; jua lisichiwe na uchugu wenu bado kukutokeni;


Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.


Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki nikasema, Ni watu waliopotoka mioyo hawa; hawakujua njia zangu;


Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo