Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 2:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Marra wakakusanyika watu wengi isibaki nafasi hatta mlangoni: akasema nao neno lake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekana mlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekana mlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, wakaja watu wengi sana hata nafasi yoyote ikakosekana mlangoni. Yesu alikuwa akiwahubiria ujumbe wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Watu wengi wakakusanyika, kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Hivyo watu wengi wakakusanyika kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno.

Tazama sura Nakili




Marko 2:2
20 Marejeleo ya Msalaba  

akafunua kinywa chake, akawafundisha, akinena,


Hatta baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiikhubiri injili ya ufalme wa Mungu,


Na mji wote nlikuwa umekusanyika mlangoni.


wakamwona, wakamwambia, Watu wote wanakutafuta.


Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali.


AKAINGIA Kapernaum tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.


Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, makutano yote wakamwendea, akawafundisha.


Yesu aliposhuka chomboni, akaona makutano mengi, akawahurumia, kwa sababu walikuwa kana kondoo wasio mchunga; akaanza kuwafundisha mengi.


HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.


Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya.


IKAWA muda si muda alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji, akikhutubu na kukhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu. Na wale thenashara walikuwa pamoja nae,


Na mfano ndio huu: Mbegu ni neno la Mungu.


Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao.


Na baada ya kukhubiri katika Perga wakatelemka hatta Attalia.


Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia.


Nao walipokwisha kushuhudia na kulikhubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemi wakaikhubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.


Lakini yasemaje? Lile neno ni karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani ni lile neno la imani tulikhubirilo;


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo