Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Yesu aliposikia akawaambia, Wenye afya hawabitaji tabibu bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dbambi wapate kutubu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Yesu alipowasikia, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Yesu alipowasikia, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Yesu alipowasikia, akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Isa aliposikia haya akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Isa aliposikia haya akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Tazama sura Nakili

Marko 2:17
21 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.

Akamjibu baba yake akamwambia, Tazama, mimi nimekutumikia hii miaka mingapi: wala sikukhalifu amri yako wakati wo wote wala hukunipa mimi mwana mbuzi wakati wo wote illi nifurahi pamoja na rafiki zangu.

Nawaambieni, Kadhalika itakuwako furaha mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tissa na tissaini, wasiohitaji toba.

Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.

Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.

Wakajibu, wakamwambia, Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufuudisha sisi? Wakamtoa nje.

Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nae wakasikia haya, wakamwambia, Je! sisi nasi tu vipofu?

nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.

aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo