Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 2:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Akaondoka marra, akajitwika kitanda chake, akatoka mbele yao wote; hatta wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakinena, Namna hii hatujapata kuyaona kamwe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Mara, watu wote wakiwa wanamtazama, huyo mtu akainuka, akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watu wote wakashangaa na kumtukuza Mungu wakisema, “Hatujapata kamwe kuona jambo kama hili.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Mara, watu wote wakiwa wanamtazama, huyo mtu akainuka, akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watu wote wakashangaa na kumtukuza Mungu wakisema, “Hatujapata kamwe kuona jambo kama hili.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Mara, watu wote wakiwa wanamtazama, huyo mtu akainuka, akauchukua mkeka wake, akaenda zake. Watu wote wakashangaa na kumtukuza Mungu wakisema, “Hatujapata kamwe kuona jambo kama hili.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!”

Tazama sura Nakili

Marko 2:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

Makutano wote wakashangaa wakasema, Huyu siye mwana wa Daud?

hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.

Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.

Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii!

Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako.

Akaweka mikono yake juu yake, akanyoka marra hiyo, akaanza kumtukuza Mungu.

Mmoja wao akiona ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo.

Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.

Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?

Tangu awali haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu aliyezaliwa hali hii.

Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:

Tufuate:

Matangazo

Matangazo