Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 2:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAINGIA Kapernaum tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Baada ya siku kadhaa, Yesu alirudi Kafarnaumu, watu wakapata habari kwamba alikuwa nyumbani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Baada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba yupo nyumbani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Baada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani.

Tazama sura Nakili




Marko 2:1
13 Marejeleo ya Msalaba  

akatoka Nazareti, akaenda, akakaa Kapernaum, ulioko pwani, mipakani mwa Zabulon na Nafthalim:


AKAPANDA chomboni, akavuka, akafika mjini kwake.


Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali.


Marra wakakusanyika watu wengi isibaki nafasi hatta mlangoni: akasema nao neno lake.


Kiisha wakaingia nyumbani; makutano wakakusanyika tena, wao wenyewe wasiweze kula hatta mkate.


Hatta alipoingia nyumbani, amewaacha makutano, wanafunzi wake wakamwuliza khabari za ule mfano.


Akaondoka huko, akaenda zake hatta mipaka ya Turo na Sidon. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kustirika.


Hatta alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza?


Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia methali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako: mambo yote tuliyosikia yametendeka Kapernaum, yatende na hapa pia katika inchi yako mwenyewe.


Na kumbe! watu wanachukua mtu kitandani mwenye kupooza: wakitaka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.


Huyu aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Yahudi hatta Galilaya, akamwendea, akamsihi ashuke akamponye mwana wake; kwa maana alikuwa kufani.


Bassi sauti hii ilipokuja makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa killa mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo