Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 16:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo wabaya saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo wabaya saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo wabaya saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Isa alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, aliyekuwa amemtoa pepo wachafu saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Isa alipofufuka alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Maria Magdalene, yule ambaye alikuwa amemtoa pepo wachafu saba.

Tazama sura Nakili




Marko 16:9
12 Marejeleo ya Msalaba  

Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yose, na mama yao wana wa Zebedayo.


Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; katika hawa alikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama wa Yakobo mdogo na wa Yose, na Salome:


Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yose wakapatazama alipowekwa.


Wakatoka humo, wakakimbia kutoka kaburini: kwa maana waliingia tetemeko na ushangao: wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.


Na hao waliowaambia mitume mambo haya ni Mariamu Magdalene, na Yoanna, na Mariamu mama yake Yakobo na wengine waliokuwa pamoja nao.


na wanawake kadha wa kadha waliokuwa wameponywa pepo wabaya na magonjwa, Mariamu aliyeitwa Magdalene, aliyetokwa na pepo saba,


akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani, na mmoja miguuni, hapo ulipowekwa mwili wa Yesu.


Hatta siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walipokusanyika illi kumega mkate, Paolo akawakhutubu, akaazimu kusafiri siku ya pili yake, akafuliza maneno yake mpaka nsiku wa manane.


Siku ya kwanza ya juma killa mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; changizo zisifanyike hapo nitakapokuja:


Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo