Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 16:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 watashika nyoka kwa mikono yao; na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 watashika nyoka kwa mikono yao; na hata wakinywa kitu chochote cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.”

Tazama sura Nakili




Marko 16:18
21 Marejeleo ya Msalaba  

akimsihi sana, akinena. Binti yangu mdogo yu katika kufa: nakuomba nje, nweke mkono wako juu yake, apate kupona, nae ataishi.


Tazameni, nawapeni mamlaka va kuwakanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hapana kitu kitakachowadhuru ninyi kamwe.


hatta wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizogusa mwili wake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.


Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi?


Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini.


ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.


Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya: ondoka, ukatandike kitanda chako.


Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


mwingine imani katika Roho yule yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo