Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 16:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Baadae akaonekana na wale edashara walipokuwa wakila, akawalaumu kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki waliomwona alipofufuka.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mwishowe Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya kutoamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaamini wale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mwishowe Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya kutoamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaamini wale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mwishowe Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya kutoamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaamini wale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Baadaye Isa akawatokea wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakila chakula. Akawakemea kwa kutoamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao kwa kutosadiki wale waliomwona baada yake kufufuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Baadaye Isa akawatokea wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakila chakula. Akawakemea kwa kutoamini kwao na kwa ugumu wa mioyo yao kwa kutosadiki wale waliomwona baada yake kufufuka.

Tazama sura Nakili

Marko 16:14
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka.

Akawaambia, Hivi na ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kuwa killa kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia najis;

Maneno yao yakaonekana kuwa ni upuzi kwao, wala hawakuwasadiki.

Nae akawaambia, Enyi wapumbavu, na wenye mioyo mizito katika kuyaamini yote waliyoyasema manabii!

Bassi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Nisipoona mikononi mwake alama za misumari, na kutia kidole changu katika alama za misumari, na kutia mkono wangu uhavuni mwake, sitaamini kabisa.

Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo ndani marra ya pili, na Tomaso pamoja nao. Yesu akaja, milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani kwenu.

Akiisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako, ukatazame mikono yangu; kalete mkono wako, uutie katika ubavu wangu; wala nsiwe asiyeamini, bali aaminiye.

BAADA ya haya Yesu alijionyesha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia; nae alijionyesha hivi.

Hii ndiyo marra ya tatu Yesu alionekana na wanafunzi wake baada ya kufufuka katika wafu.

na baada ya kuteswa kwake, akawadhihirisbia ya kwamba yu hayi, kwa dalili nyingi, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyonkhusu ufalme wa Mungu.

na ya kuwa alionekana na Kefa; tena na wathenashara;

Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo