Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 16:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yakobo na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Sabato ilipomalizika, Mariamu Magdalene, Mariamu mama yake Yakobo, na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Sabato ilipomalizika, Maria Magdalene, Maria mama yake Yakobo, na Salome walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Isa.

Tazama sura Nakili




Marko 16:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Nae akiwapo Bethania, nyumbani mwa Simon mwenye ukoma, ameketi chakulani, akaja mwanamke mwenye kibweta cha alabastro cha marhamu ya hali udi, safi, ya thamani nyingi; akakivunja kibweta cha alabastro akaimimina kichwani pake.


Ametenda alivyoweza; amenipaka mwili marhamu kwa ajili ya maziko yangu.


Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; katika hawa alikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama wa Yakobo mdogo na wa Yose, na Salome:


Hatta ikiisba kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato,


Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yose wakapatazama alipowekwa.


Hatta assubuhi mapema, siku ya kwanza ya sabato, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza;


Wakatoka humo, wakakimbia kutoka kaburini: kwa maana waliingia tetemeko na ushangao: wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.


Ilikuwa siku ya Maandalio, sabato ikawadia.


Na siku ya sabato wakastarehe kama ilivyoamriwa.


HATTA siku ya kwanza ya juma, ikianza kupambazuka, wakaenda kaburini wakiyaleta yale manukato waliyoyaweka tayari, na wengine pamoja nao.


Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.


Bassi Wayahudi, kwa maana ni Maandalio, miili isikae juu va msalaba siku ya sabato (maana siku ya sabato ile ilikuwa siku kuhwa), wakamwomba Pilato, miguu yao ivunjwe, wakaondolewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo