Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 15:43 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

43 akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Arimathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila woga, akaomba apewe mwili wa Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Arimathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila woga, akaomba apewe mwili wa Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Arimathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila woga, akaomba apewe mwili wa Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na alikuwa anautarajia ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na ambaye alikuwa anautarajia Ufalme wa Mwenyezi Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Isa.

Tazama sura Nakili




Marko 15:43
16 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho, wa kwanza.


Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza wa mwisho: maana waitwao wengi, hali wateule wachache.


Ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusuf, nae mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;


Petro akamfuata mbali, hatta ndani katika behewa ya kuhani mkuu; akaketi pamoja na watumishi, anakota moto.


Pilato akastaajabu, kwa sababu amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo.


Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi.


Akatoka mtu, jina lake Yusuf, nae ni mtu wa baraza yao, mtu mwema, mwenye haki


(mtu huyu hakuwa akikubali shauri lao wala tendo lao), mwenyeji wa Arimathaya, mji wa Wayahudi, nae mwenyewe akiutazamia ufalme wa Mungu.


Hatta baada ya haya, Yusuf, aliye wa Arimathaya, nae vu mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri (maana aliwaogopa Wayahudi), akamwomba Pilato rukhusa auondoe mwili wake Yesu: Pilato akampa rukhusa. Bassi akaenda akauondoa mwili wake.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


Wafu wengi wakaamini miongoni mwao, nao wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.


Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo