Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 15:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Nao waliosulibiwa pamoja nae wakamlaumu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Ati yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke kutoka msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Ati yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke kutoka msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Ati yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke kutoka msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Basi huyu Al-Masihi, huyu mfalme wa Israeli, ashuke sasa msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Basi huyu Al-Masihi, huyu Mfalme wa Israeli, ashuke sasa kutoka msalabani, ili tupate kuona na kuamini.” Wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.

Tazama sura Nakili




Marko 15:32
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi vizazi vyote tangu Ibrahimu hatta Daud vizazi kumi na vine; na tangu Daud hatta uhamisho ule wa Babel vizazi kumi na vine; na tangu uhamisho ule wa Babel hatta Kristo vizazi kumi na vine.


Aliponya watu wengine, hawezi kujiponya nafsi yake. Akiwa mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani, naswi tutamwamini.


Vilevile wa ayangʼanyi nao waliosulibiwa pamoja nae walimshutumu.


Anwani ya mshitaka wake iliandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDU.


Na pamoja nae walisulibi wanyangʼanyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto.


Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabbi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israeli.


wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli.


Ni nini, bassi, ikiwa hawakuamini wengine? Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?


walioikosa kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, nao waipindua imani ya watu wengine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo