Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 15:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Pilato akapenda kuwafanyia radhi makutano, akawafungulia Barabba: akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, asulibiwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Pilato, akitaka kuridhisha umati ule wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Isa apigwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Pilato, akitaka kuuridhisha ule umati wa watu, akawafungulia Baraba. Naye baada ya kuamuru Isa achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe.

Tazama sura Nakili




Marko 15:15
17 Marejeleo ya Msalaba  

na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.


Ndipo akawafungulia Barabba: na alipokwisha kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa apate kusulibiwa.


na watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa mataifa, nao watamdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumtemea mate, na kumwua: na siku ya tatu atafufuka.


Pilato akawaambia, Kwani, ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulihishe.


na wakiisha kumpiga mijeledi, watamwua; na siku ya tatu atafufuka.


Bassi nikiisha kumrudi, nitamfungua.


BASSI ndipo Pilato akamtwaa Yesu, akampiga mijeledi.


Bassi ndipo akamtia mikononi mwao asulibishwe. Bassi wakampokea Yesu:


Na miaka miwili ilipotimia. Feliki akampokea Porkio Festo atawale badala yake. Na Feliki, akitaka kuwafanyia Wayahudi fadhili, akamwacha Paolo amefungwa.


Lakini Festo akitaka kujipendekeza kwa Wayahudi akamjibu Paolo, akisema, Wataka kwenda Yerusalemi, ukahukumiwe huko mbele yangu?


Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana.


yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo