Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 15:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Pilato akawaambia, Kwani, ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulihishe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya ubaya gani?” Lakini wao wakazidi kupaza sauti, “Msulubishe!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya ubaya gani?” Lakini wao wakazidi kupaza sauti, “Msulubishe!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya ubaya gani?” Lakini wao wakazidi kupaza sauti, “Msulubishe!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele zaidi, wakisema, “Msulubishe!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Pilato akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, wakisema, “Msulubishe!”

Tazama sura Nakili




Marko 15:14
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.


akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Wakapiga kelele tena, Msulibishe.


Pilato akapenda kuwafanyia radhi makutano, akawafungulia Barabba: akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, asulibiwe.


Nao wakalia, wakisema, Msulibishe, msulibishe.


Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu.


Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa.


Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.


Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani? Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake.


Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake.


Na wasipopata sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe.


Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu.


Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo