Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 14:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Nao wakiisha kuketi chakulani, wakila, Yesu akasema, Amin, nawaambieni, mmoja wenu, nae anakula pamoja nami, atanisaliti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Walipokuwa mezani wakila, Yesu alisema, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Walipoketi mezani wakila, Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Walipoketi mezani wakila, Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”

Tazama sura Nakili




Marko 14:18
36 Marejeleo ya Msalaba  

Walipokuwa wakila, akasema, Amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.


Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.


Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali nfalme wa Mungu kama mtoto mchanga hatauingia kabisa.


Yesu akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, Hapana mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume au ndugu wake, au baba, au mama, au mke, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, au kwa ajili ya Injili,


Ilipokuwa jioni yuaja pamoja na wathenashara.


Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia, mmoja mmoja, Ni mimi? na mwingine, Ni mimi?


Amin, nawaambieni, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hatta siku ile nitakaponnywa mpya katika ufalme wa Mungu.


Amin, nawaamhieni, Killa ikhubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.


Amin, nawaambieni, Dbambi zote watasamehewa wana Adamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;


Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao.


Akaugua rohoni mwake, akanena, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.


AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.


Kwa kuwa ye yote atakaewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa kuwa ninyi watu wa Kristo, amin nawaambieni hatakosa thawabu yake.


tangu damu ya Habil hatta damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhhahu na patakatifu. Naam, nawaambieni, itatakwa kwa kizazi hiki.


Illa angalieni, mkono wake anisalitiye u pamoja nami mezani.


Akawaambia, Amin, nawaambieni, Hapana nabii apatae kukubaliwa katika inchi yake mwenyewe.


Akamwambia, Amin, amin, nakuambieni, Tangu sasa mtaziona mbingu zimefunguka, na malaika wa Mungu wakipanda, wakishuka juu ya Mwana wa Adamu.


Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.


Alipokwisha kusema haya, Yesu akafadhaika rohoni, akashuhudu, akinena, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.


Wanafunzi wakatazamana, wakiona mashaka, ni nani anaemtaja,


Yesu akamjibu, Je! uzima wako utauweka kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hatta utakapokuwa umenikana marra tatu.


Amin, amin, nakuambia, Ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga, ukienda ulikotaka; utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakufunga, atakuchukua usikotaka.


Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.


Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate, mkashiba.


Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa mkate ule kutoka mbinguni, bali Baba yangu anawapa mkate ule utokao mbinguni ulio wa kweli.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi ana uzima wa milele.


Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo