Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 13:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme utapigana na ufalme: kutakuwa na matetemeko ya inchi mahali mahali; kutakuwa na njaa, na fitina: Hayo ndio mwanzo wa utungu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali na njaa. Haya yatakuwa ndio mwanzo wa uchungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na mitetemeko sehemu mbalimbali na njaa. Haya yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

Tazama sura Nakili

Marko 13:8
21 Marejeleo ya Msalaba  

Haya yote ni mwanzo wa utungu.

Tena mtakaposikia vita na khabari za vita, msitishwe: maana hayana buddi kutukia, lakini mwisho wenyewe bado.

Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.

Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.

Maana wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo niwenye mimba; nao hawataokolewa.

Akatoka farasi mwingine mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katikii inchi, watu wauawe, akapewa upanga mkubwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo