Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 12:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Daud mwenyewe amwita Bwana: bassi amekuwaje mwana wake? Na ule mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 “Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 “Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 “Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanawe?” Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Umati ule wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.

Tazama sura Nakili




Marko 12:37
14 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana, Na watamwita jina lake Immanuel; tafsiri yake, Mungu kati yetu.


Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Makuhani wakuu na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, wakatambua ya kuwa anawanena wao.


Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.


nao bawakuona la kutenda; maana watu wote waliambatana nae, wakimsikiliza.


Watu wote wakaamka mapema wakamwendea alfajiri mle hekaluni illi kumsikiliza.


Bassi kundi kubwa la Wayuhudi walijua ya kuwa yeye yuko huko; wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, bali wamwone na Lazaro, ambae alimfufua katika wafu.


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo