Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 12:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Wakamwendea, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?

Tazama sura Nakili

Marko 12:14
36 Marejeleo ya Msalaba  

Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu.

Bassi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, au si halali?

Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodiano, illi wamnase kwa maneno.

Nae, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? nileteeni dinari niione. Wakaleta.

Alipokuja, marra akamwendea, akasema, Rabbi, Rabbi; akambusu sana.

Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo?

Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona mtu huyu amipotosha taifa letu, anawakataza watu wasimpe Kaisari kodi, akisema ya kwamba yeye mwenyewe yu Kristo, mfalme.

Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.

Kwa sababu hiyo tena mwatoa kodi; kwa kuwa wao ni watumishi wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyohiyo.

Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.

Maana mimi nikiwatia huzuni, hassi ni nani anifurahishae illa yeye ahuzunishwae nami?

KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei;

Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia.

Hatta imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awae yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemjua Kristo kwa jinsi ya mwili, sasa lakini hatumjui hivi tena.

Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.

Lakini wale wenye sifa kwamba wana cheo, walivyo vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwana Adamu—nasema, wale wenye sifa hawakuniongezea kitu,

bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuaminiwe Injili ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wana Adamu bali Mungu anaetupima mioyo yetu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo