Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 12:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAANZA kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akazungusha nzio, akachimbia shimo lake shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Yesu alianza kusema nao kwa mifano: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Isa akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, na ndani yake akachimba shimo la shinikizo la kukamulia zabibu, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri hadi nchi nyingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Isa akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akachimba shimo ndani yake kwa ajili ya shinikizo la kusindika divai, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwenda nchi nyingine.

Tazama sura Nakili




Marko 12:1
38 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema nao mengi kwa mifano, akinena, Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu.


Mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda kufanya kazi katika shamba langu la mizabibu.


Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.


Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumishi wake kwa wale wakulima, wajiokee matunda yake.


Maana ni mfano wa mtu atakae kusafiri kwenda inchi ya ugeni, aliwaita watumishi wake, akaweka kwao mali zake.


Wakamjibu Yesu, wakanena, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi kwa mamlaka gani nitendayo haya.


Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe.


Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumfukuza Shetani?


Akawafundisha mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake,


Hatta baada ya siku si nyingi yule mdogo akakusanya vitu vyake vyote, akasafiri kwenda inchi ya mbali: akatapanya huko mali zake kwa maisha ya uasharati.


Bassi akasema, Mtu mmoja, mungwana, alisafiri kwenda inchi ya mbali illi kujipatia ufalme na kurejea.


Wakamwambia, Wapi utakapo tuiandalie?


Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue.


Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo