Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 11:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 maana haukuwa wakati wa tini. Yesu akajibu, akauambia, Tangu leo hatta milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Hapo akauambia mtini, “Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda kwako.” Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.

Tazama sura Nakili




Marko 11:14
15 Marejeleo ya Msalaba  

Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake illa majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hatta milele. Mtini ukauyauka marra moja.


Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.


Nae aangukiae juu ya jiwe hili atavunjikavunjika: nae amhae litamwangukia, litampondaponda.


Nalo shoka limekwisha kuwekwa penye shina la miti; bassi killa mti usiozaa matunda mazuri unakatwa na kutupwa motoni.


Killa mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.


Akaona toka mbali mtini wenye majani, akaenda illi labuda aone kitu juu yake: na alipofika hakuona kitu illa majani:


Wakafika Yerusalemi, Yesu akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadilio fedha, na viti vyao wauzao njiwa;


Mtu asipokaa ndani yangu, atupwa nje kama tawi, akauka; huyakusanya, huyatupa motoni, yakateketea.


Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.


Mwenye kudhulumu na atende dhuluma tena; na mwenye uchafu na awe mchafu tena, na mwenye haki na afanye haki tena, na mtakatifu na atakaswe tena.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo