Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 10:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 illa atapewa marra mia sasa wakati huu, nyumba na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na mateso: na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa: Nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa: Nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa: nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili




Marko 10:30
32 Marejeleo ya Msalaba  

Na killa mtu atakaenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakaenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ntakaokuwa.


nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikazaa, hizi mia, hizi sittini, hizi thelathini.


Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa.


illa atapokea zaidi marra nyingi sasa wakati huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.


Na Yesu alikuwa akitembea ndani ya hekalu, katika ukumbi wa Sulemani.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu,


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa.


Lakini utawa pamoja na kuridhia ni faida nyingi.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.


Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.


FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo