Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 10:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, kwa shidda gani wenye kuitegemea mali wataingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, “Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika ufalme wa Mungu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Isa akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Wanafunzi wake wakashangazwa sana na maneno hayo. Lakini Isa akawaambia tena, “Wanangu, tazama jinsi ilivyo vigumu kwa wale wanaotumainia mali kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Marko 10:24
28 Marejeleo ya Msalaba  

Wanafunzi wake waliposikia, wakashangaa sana, wakinena, Nani bassi awezae kuokoka?


Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii!


Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Kwa shidda gani wenye mali wataingia katika ufalme wa Mungu!


Mafarisayo nao wakayasikia haya yote, nao walikuwa wakipenda fedha; wakamdhihaki.


Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi.


Bassi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, Hapana.


Bassi watu wengi katika wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, Neno hili ni gumu, nani awezae kulisikia?


Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.


Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha;


WATOTO wangu wadogo, nawaandikia haya illi msitende dhambi. Na ijapo mtu akatenda dhambi tuna Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,


Ninyi, watoto wangu, mwatokana na Mungu: nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


Watoto wangu wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.


Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u maskini, na mtu wa kuhurumiwa, na mhitaji, na kipofu, na nchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo