Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 10:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha uje unifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Isa akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Isa akamtazama na kumpenda, akamwambia, “Umepungukiwa na kitu kimoja. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho uwape maskini hizo fedha, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Tazama sura Nakili




Marko 10:21
29 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.


Walakini yeye akakunja uso kwa neno lile, akaenda zake kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.


Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu ameichagua sehemu iliyo njema, ambayo hataondolewa.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Nae alipokaribia akauona mji, akaulilia,


Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja.


Na kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu: ingawa nizidipo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?


Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa.


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Maana mtu awae yote atakaeishika sharia yote, na pamoja na hayo, akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.


Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.


Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Lakini nina neno jun yako, kwa sababu umeacha npendo wako wa kwanza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo