Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 10:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Usidanganye, Waheshimu haha yako na mama yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Unazijua amri: ‘Usizini, Usiue, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Unazijua amri: ‘Usizini, Usiue, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Unazijua amri: ‘Usizini, Usiue, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, usidanganye, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

Tazama sura Nakili




Marko 10:19
16 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu.


Wazijua amri, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Waheshimu baba yako na mama yako.


Maana ile, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishududu uwongo, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani wako kama nafsi yako.


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Niambieni, ninyi ninaotaka kuwa chini ya sharia, hamwisikii torati?


Maana sharia yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, alisema, Usiue, pia. Bassi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sharia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo