Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 10:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanyeje niupate uhai wa milele?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Isa alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Isa alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

Tazama sura Nakili




Marko 10:17
28 Marejeleo ya Msalaba  

Nao walipoufikia mkutano, mtu akamjia, akampigia magoti, akinena,


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari.


Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.


Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu.


Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe?


Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena.


Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele?


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


kiisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?


Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Lakini simama, uingie mjini, utaambiwa yatakayokupasa kutenda.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.


Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?


tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,


Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo