Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 10:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Lakini Yesu alipoona akachukiwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wachanga waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawo ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Isa alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Isa alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mwenyezi Mungu ni wa wale walio kama hawa.

Tazama sura Nakili




Marko 10:14
36 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


Bassi, ye yote anyenyekeae kama kitoto hiki, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.


Lakini Yesu akasema, Waacheni vitoto, wala msiwakataze kuja kwangu; kwa maana walio mfano wa hawo, ufalme wa mbinguni ni wao.


Wa kheri wateswao kwa ajili ya haki: maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:


Akageuka akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akinena, Enenda zako nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, hali ya wana Adamu.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu.


Ninyi m watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.


Tʼena malimbuko yakiwa matakatifu, vivyo hivyo na, donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo vivyo hivyo.


Bassi kwa khabari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu, bali kwa khabari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya haha zetu.


Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa kwa mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa kwa mumewe; kama isingekuwa bivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.


Mwe na ghadhabu, wala msifanye dhambi; jua lisichiwe na uchugu wenu bado kukutokeni;


nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo.


na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;


Na katika vinywa vyao haikuonwa bila. Maana hawana mawaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo