Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Marko 1:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Wakashangaa wote hatta wakaulizana, wakinena, Nini hii? Elimu hii mpya ni elimn gani? Maana kwa mamlaka awaamuru pepo wachafu nao wakamtii!

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Watu wote wakashangaa, wakaulizana, “Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Watu wote wakashangaa, wakaulizana, “Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Watu wote wakashangaa, wakaulizana, “Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”

Tazama sura Nakili

Marko 1:27
15 Marejeleo ya Msalaba  

hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.

Yule pepo mchafu akamrarua, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.

Khahari zake zikaenea marra inchi zote kando ya Galilaya.

Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, kwa shidda gani wenye kuitegemea mali wataingia katika ufalme wa Mungu!

Wakawa njiani, wakipanda kwenda Yerusalemi; na Yesu alikuwa akiwatangulia: wakashangaa, na wakifuata wakaogopa. Akawachukua tena wale thenashara akaanza kuwaambia khabari za mambo yatakayompata, akinena,

Na wakiingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe: wakastaajabu.

Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka.

Ametenda yote vizuri; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.

Ushangao ukawashika wote, wakaambiana wao kwa wao, wakinena, Neno gani hili, maana kwa mamlaka na uweza awaamuru pepo wachafu, nao watoka?

AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi.

Wakamshika, wakamchukua hatta Areopago, wakisema, Je, twaweza kujua maana ya elimu hii mpya inenwayo nawe?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo