Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 9:56 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

56 Maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za wana Adamu, bali kuziokoa. Wakaenda zao hatta mji mwingine.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

56 Wakatoka, wakaenda kijiji kingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

56 Wakatoka, wakaenda kijiji kingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

56 Wakatoka, wakaenda kijiji kingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

56 Naye Isa na wanafunzi wake wakaenda kijiji kingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

56 nao wakaenda kijiji kingine.

Tazama sura Nakili




Luka 9:56
16 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.


kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.


Yesu akajibu, akasema, Acheni kadiri hii. Akamgusa sikio, akamponya.


Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.


Akageuka, akawakaripia, akasema, Hamjui ni moyo wa namna gani mlio nao.


Na walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja akamwambia, Nitakufuata ko kote uendako, Bwana.


Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele.


Na mtu akisikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.


Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo