Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 9:51 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

51 Ikawa siku za kupandishwa kwake juu zilipokuwa karibu kutimia, yeye mwenyewe akauelekeza nso wake kwenda Yerusalemi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

51 Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye alikata shauri kwenda Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

51 Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye alikata shauri kwenda Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

51 Wakati ulipokaribia ambapo Yesu angechukuliwa juu mbinguni, yeye alikata shauri kwenda Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

51 Wakati ulipokaribia wa yeye kuchukuliwa mbinguni, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

51 Wakati ulipokaribia wa yeye kuchukuliwa mbinguni, alikaza uso wake kwenda Yerusalemu.

Tazama sura Nakili




Luka 9:51
29 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Nina ubatizo wa kubatizwa nao, na nina dhiiki namna gani hatta utakapotimizwa!


Akawa akizungukazunguka katika miji ni vijiji, akifundisha, na kufanya safari kwenda Yerusalemi.


Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemi, alikuwa akipita kati ya Samaria na Galilaya.


Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii.


Nao wakisikia haya akaongeza akawaambia mfano, kwa sababu alikuwa akikaribia Yerusalemi, nao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana marra moja.


Alipokwisha kusema haya, akaendelea mbele, akipanda kwenda Yerusalemi.


Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni.


Na walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja akamwambia, Nitakufuata ko kote uendako, Bwana.


HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo.


Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba.


Lakini sasa nakwenda zangu kwake aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizae, Unakwenda zako wapi?


Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi.


Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza?


hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu:


Akiisha kusema haya, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.


aliyotenda katika Kristo alipomfufua, akamweka mkono wake wa kuume katika mbingu,


nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo