Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 9:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Watu wakikataa kuwakaribisha, tokeni katika mji huo, nanyi mnapotoka kung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”

Tazama sura Nakili




Luka 9:5
13 Marejeleo ya Msalaba  

nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.


Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao.


Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.


Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.


Akamwagiza asimwambie mtu: illa enenda, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe kwa kutakasika kwako alivyoamuru Musa, illi kuwa ushuhuda kwao.


Na nyumba yo yote mtakayoingia, kaeni humo, katokeni humo.


akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.


Nao wakawakungʼutia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo