Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 9:48 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

48 akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 akawaambia, “Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 akawaambia, “Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 akawaambia, “Mtu yeyote anayempokea mtoto huyu mdogo kwa jina langu, ananipokea mimi; na yeyote anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma. Maana yule aliye mdogo kuliko wote kati yenu ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Kisha akawaambia, “Yeyote amkaribishaye mtoto huyu mdogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi, na yeyote atakayenikaribisha mimi, atakuwa amemkaribisha yeye aliyenituma. Kwa maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu, ndiye aliye mkuu kuliko wote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Luka 9:48
23 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni mmoja wa wadogo hawa apotee.

Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.

Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

Nae atawajibu, akinena, Amin, nawaambieni, Kadiri msivyomtendea mmojawapo katika hawo walio wadogo, na mimi hamkunitendea.

Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.

Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.

Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.

Lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa wenu awe kama aliye mdogo; nafe atanguliae kama akhudumuye.

mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na kuketi katika viti vya enzi, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.

Maana nawaambieni, Katika wazao wa wanawake hapana nabii aliye mkuu kuliko Yobana Mbatizaji: lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.

Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.

Aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendae; nae anipendae atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda, na kujidhihirisha kwake.

Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.

Bassi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, awakweze kwa wakati wake;

Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo.

Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo