Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 9:44 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

44 Yawekeni maneno haya masikioni mwenu: kwa maana Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

44 “Tegeni masikio, muyasikie mambo haya: Mwana wa Mtu anakwenda kutiwa mikononi mwa watu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

44 “Tegeni masikio, muyasikie mambo haya: Mwana wa Mtu anakwenda kutiwa mikononi mwa watu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

44 “Tegeni masikio, muyasikie mambo haya: Mwana wa Mtu anakwenda kutiwa mikononi mwa watu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

44 “Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

44 “Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu.”

Tazama sura Nakili




Luka 9:44
26 Marejeleo ya Msalaba  

Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa.


Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.


Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akiwaambia ya kwamba Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hatta akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka.


Na wote waliosikia wakayaweka mioyoni mwao, wakinena, Mtoto gani bassi atakuwa huyu? Kwa maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nae?


Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii.


Bali Mariamu aliyahifadhi maneno haya yote akiyatafakari moyoni.


Akashuka pamoja nao, akafika Nazareti, akawa anawatii: mama yake akayahifadhi maneno haya yote moyoni mwake.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


Yesu akawajihu, Sasa hivi mnaamini?


Lakini nimewaambieni haya, illi kusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambieni. Haya sikuwaambieni tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwa pamoja nanyi.


Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.


mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:


KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo