Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 9:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Ikawa hawo walipokuwa wakijitenga nae, Petro akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa: na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, kimoja cha Eliya: nae hajui asemalo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Basi, watu hao wawili walipokuwa wakiondoka, Petro alimwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa! Basi, tujenge vibanda vitatu: Kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Elia.” Kwa kweli hakujua anasema nini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Basi, watu hao wawili walipokuwa wakiondoka, Petro alimwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa! Basi, tujenge vibanda vitatu: Kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Elia.” Kwa kweli hakujua anasema nini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Basi, watu hao wawili walipokuwa wakiondoka, Petro alimwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa! Basi, tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Elia.” Kwa kweli hakujua anasema nini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Musa na Ilya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Isa, “Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya.” Lakini Petro hakujua alichosema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Musa na Ilya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Isa, “Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya.” Lakini Petro alikuwa hajui asemacho.

Tazama sura Nakili




Luka 9:33
13 Marejeleo ya Msalaba  

Nao walipoufikia mkutano, mtu akamjia, akampigia magoti, akinena,


Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka tutafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.


Yesu akawaambia, Hamjui mnaioliomba. Mnaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, na kubatizwa nbatizo nibatizwao mimi?


Simon akajibu, akasema, Bwana, tulisumbuka usiku kucha, tusipate kitu: illakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.


Hatta alipokuwa akisema haya likawako wingu, likawatia uvuli; wakaogopa walipoingia katika lile wingu.


Yohana akajibu, akasema, Mwalimu, tulimwona mtu anafukuza pepo kwa jina lako, tukamkataza kwa kuwa hatufuati sisi.


Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, yatutosha.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo