Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 9:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Akawaambia, Msichukue kitu cha njiani, fimbo wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala msiwe na kanzu mbili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Akawaambia, “Mnaposafiri msichukue chochote: Msichukue fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala hata koti la ziada.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Akawaambia, “Mnaposafiri msichukue chochote: Msichukue fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala hata koti la ziada.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Akawaambia, “Mnaposafiri msichukue chochote: msichukue fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala fedha, wala hata koti la ziada.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.

Tazama sura Nakili




Luka 9:3
12 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaita wale thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili; akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu:


Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni: wala miili yenu mvaeni.


Bassi ikiwa Mungu huvika hivi haya majani ya kondeni yaliyopo leo, yakatupwa kalibuni kesho, si ninyi zaidi sana, enyi wa imani haba?


Akawaambia, Nilipowatuma bila mifuko na mkoba na viatu, mlipunguka kitu? Wakasema, Hapana.


Akajibu akawaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe yeye asiye nayo, na mwenye vyakula, na afanye vivyo hivyo.


Nae Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake: na palikuwa na kundi kubwa la watoza ushuru, na watu wengine waliokuwa wameketi pamoja nao chakulani.


Na nyumba yo yote mtakayoingia, kaeni humo, katokeni humo.


Hakuna mfanya vita ajitiae katika shughuli za dunia; illi ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo