Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 9:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Hatta jua lilipoanza kuchwa wale thenashara wakamwendea wakamwambia, Uwaage makutano illi waende zao hatta vijiji vilivyo kandokando na mashamba wakapate mahali pa kulala na vyakula: maana hapa tulipo nyika tupu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage watu hawa ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”

Tazama sura Nakili

Luka 9:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu aliposikia, akatoka huku katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, kwa faragha. Na makutano waliposikia, wakamfuata kwa miguu toka miji yao.

Nae hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakinena. Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.

Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia makutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, hawana kitu cha kula: na kuwaaga wakifunga sitaki, wasije wakazimia njiani.

Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa.

Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki mbili, tusipokwenda sisi wenyewe tukawannnulie vyakula watu hawa wote.

BAADA ya haya Yesu alikwenda zake ngʼambu ya bahari ya Galilaya, bahari ya Tiberia.

Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokofu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho ya Yesu Kristo,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo