Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 8:47 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

47 Yule mwanamke alipoona ya kuwa hakustirika, akaja akitetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu hatta akamgusa, na jinsi alivyoponywa marra moja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

47 Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

47 Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

47 Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara.

Tazama sura Nakili




Luka 8:47
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari.


Na yule mwanamke akaingiwa na khofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.


Yesu akasema, Mtu alinigusa, kwa kuwa naliona nguvu zimenitoka.


Akamwambia. Jipe moyo mkuu, binti, imani yako imekuponya; enenda zako kwa amani.


Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila;


Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na khofu na matetemeko mengi.


Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa khofu na kutetemeka.


Bassi, wapendwa, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo, bali sasa zaidi mimi nisipokuwapo, utimizeni wokofu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka;


Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo