Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 8:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Na tazama, mtu mmoja jina lake Yairo akamjia: nae alikuwa mkuu wa sunagogi: akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani mwake:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Hapo akaja mtu mmoja aitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupa miguuni pa Yesu, akamwomba aende nyumbani kwake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Hapo akaja mtu mmoja aitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupa miguuni pa Yesu, akamwomba aende nyumbani kwake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Hapo akaja mtu mmoja aitwaye Yairo, ofisa wa sunagogi. Alijitupa miguuni pa Yesu, akamwomba aende nyumbani kwake,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Kisha mtu mmoja, jina lake Yairo, aliyekuwa kiongozi wa sinagogi, akaja na kuanguka miguuni mwa Isa, akimwomba afike nyumbani mwake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Kisha mtu mmoja, jina lake Yairo, aliyekuwa kiongozi wa sinagogi, akaja na kuanguka miguuni mwa Isa, akimwomba afike nyumbani kwake,

Tazama sura Nakili




Luka 8:41
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato.


akaanguka kufudifudi miguuni pake, akimshukuru; nae ni Msamaria.


Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.


kwa sababu ana binti, mwana wa pekee, umri wake amepata miaka thenashara, nae yu katika kufa. Na katika kwenda kwake makutano wakamsonga.


Alipokuwa akinena haya, mtu akaja, ametoka kwa yule mkuu wa sunagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa, usimsumbue mwalimu.


Bassi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu asingalikufa.


Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.


Na Wayunani wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sunagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Na Gallio hakuyaona mambo hayo kuwa kitu.


Na Krispo, mkuu wa sunagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi wakasikia, wakaamini, wakabatizwa.


Na kwa kuwa Ludda ulikuwa karibu na Yoppa, nao wamesikia ya kwamha Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi asikawie kuja kwao.


Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo