Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 8:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Yesu akamwuliza, akisema, Jina lako nani? Akasema, Legioni, kwa sababu pepo wengi wamemwingia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi’” – kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi’” – kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi’” — kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Legioni,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Legioni,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno.

Tazama sura Nakili




Luka 8:30
7 Marejeleo ya Msalaba  

Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu sasa hivi, akaniletea zaidi ya majeshi thenashara ya malaika?


Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla?


Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba.


Akamwambia, Jina lako nani? Akajibu, akamwambia, Jina langu Legioni: kwa kuwa tu wengi.


na wanawake kadha wa kadha waliokuwa wameponywa pepo wabaya na magonjwa, Mariamu aliyeitwa Magdalene, aliyetokwa na pepo saba,


Kwa sababu amemwamuru yule pepo mchafu kumtoka mtu yule. Maana marra nyingi amempagaa, nae akafungwa, akilindwa, na kufungwa minyororo na pingu, akavikata vile vifungo, akafukuzwa na yule pepo hatta jangwani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo