Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 8:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 na Joanna mkewe Kuza waklli wake Herode, na Susanna, na wengine wengi, waliokuwa wakimkhudumia kwa mali zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Yoana mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Yoana mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Yoana mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Yoana mkewe Kuza, msimamizi wa nyumba ya watu wa nyumbani mwa Herode; Susana; na wengine wengi waliokuwa wakimhudumia kwa mali yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Yoana mkewe Kuza, msimamizi wa nyumba ya watu wa nyumbani mwa Herode; Susana; na wengine wengi waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.

Tazama sura Nakili




Luka 8:3
19 Marejeleo ya Msalaba  

WAKATI ule Herode tetrarka alisikia khabari za Yesu,


Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo ndugu yake.


Hatta panapo siku kuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodias alicheza kati ya watu, akampendeza Herode.


Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane.


Kulipokuchwa, yule bwana wa mizabibu akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ijara yao, ukianzia wa mwisho hatta wa kwanza.


Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


Kwa maana siku zote maskini mnao pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote.


Na palikuwa na wanawake wengi huko wakitazama kwa mbali, hawo ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.


Na hao waliowaambia mitume mambo haya ni Mariamu Magdalene, na Yoanna, na Mariamu mama yake Yakobo na wengine waliokuwa pamoja nao.


Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo.


NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Watakatifu wote wawasalimu, khassa wao walio wa nyumba ya Kaisari.


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo