Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 8:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Hatta aliposhuka pwani, alikutwa na udu mmoja wa mji ule, aliyekuwa ua pepo siku nyingi, nae kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, wala hakai nyumbani illa makaburini.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Alipokuwa anashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo alimjia kutoka mjini. Kwa muda mrefu mtu huyo hakuwa anavaa nguo, wala hakuwa anaishi nyumbani bali makaburini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Alipokuwa anashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo alimjia kutoka mjini. Kwa muda mrefu mtu huyo hakuwa anavaa nguo, wala hakuwa anaishi nyumbani bali makaburini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Alipokuwa anashuka pwani, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo alimjia kutoka mjini. Kwa muda mrefu mtu huyo hakuwa anavaa nguo, wala hakuwa anaishi nyumbani bali makaburini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Isa aliposhuka kutoka mashua na kukanyaga ufuoni, alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye kwa muda mrefu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Isa aliposhuka kutoka mashua na kukanyaga ufuoni, alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye kwa muda mrefu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini.

Tazama sura Nakili

Luka 8:27
8 Marejeleo ya Msalaba  

Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, nae ndiye aliyekuwa na ile legione; wakaogopa.

Wakashuka pwani katika inchi ya Wagadareni, inayokabili Galilaya.

Alipomwona Yesu, akapiga kelele, akamwangukia, akasema kwa sauti kuu. Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuomba usiniadhibu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo