Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 8:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ng'ambo.” Basi, wakaanza safari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni twende mpaka ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka.

Tazama sura Nakili




Luka 8:22
12 Marejeleo ya Msalaba  

Marra Yesu akawalazimisha wamifunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ngʼambu, wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.


Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, akaamuru kuvuka hatta ngʼambu.


Hatta Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ngʼambu katika kile chombo, wakamkusanyikia makutano mengi: nae alikuwa kando ya bahari.


Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.


Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hatta ngʼambu.


IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti:


Na walipokuwa wakienda kwa matanga akalala usingizi. Ikashuka dharuba ya upepo juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika khatari.


Akawapa rakhusa: wale pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, lile kundi likatelemka kwa kassi gengeni, wakafa baharini.


BAADA ya haya Yesu alikwenda zake ngʼambu ya bahari ya Galilaya, bahari ya Tiberia.


Tukapanda katika merikebu ya Adramuttio iliyokuwa tayari kusafiri hatta miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedoni wa Thessalonika, akiwa pamoja nasi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo