Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 8:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Naye akasema, “Ninyi mmepewa ujuzi wa siri za ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanatazama, wasione; ingawa wanasikiliza, wasielewe.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Naye akasema, “Ninyi mmepewa kufahamu siri za Ufalme wa Mwenyezi Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanatazama, wasione; ingawa wanasikiliza, wasielewe.’

Tazama sura Nakili




Luka 8:10
24 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni.


Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu; hali wale walio nje yote huwawia kwa mifano,


illi wakitazama watazame, wasione; na wakisikia wasikie, wasifahamu; wasije wakageuka, wakasamehewa dbambi zao.


Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao, Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, Wakagenka, nikawaponya.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye.


illi wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo,


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo