Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 7:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Kwa maana Yohana Mbatizaji amekuja, hali mkate, wala hanywi divai, mkasema, Yuna pepo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: ‘Amepagawa na pepo!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: ‘Amepagawa na pepo!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: ‘Amepagawa na pepo!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali mkate wala hanywi divai, nanyi mkasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali mkate wala hanywi divai, nanyi mkasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’

Tazama sura Nakili




Luka 7:33
12 Marejeleo ya Msalaba  

Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebul, je, si zaidi wale walio nyumbani mwake?


SIKU zile akaondokea Yohana Mbatizaji akikhubiri katika jangwa ya Yahudi, akinena,


Yohana mwenyewe alikuwa na mavazi yake ya singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.


Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kimioni mwake, akila nzige na asali ya mwitu.


Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Wamefanana na watoto, waketio sokoni, wakiitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi nanyi hamkucheza, tuliomboleza, nanyi hamkulia.


Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi.


Wengi wao wakasema, Ana pepo, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


Wengine walidhihaki, wakisema, Wamelewa kwa mvinyo mpya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo